Wednesday, May 29, 2013

WANAFUNZI WAKIPIGA KURA ZA SIRI ILI KUWAFICHUA WALIMU WANAOFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI SHULENI







KATIKA hali isiyo ya kawaida, wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyasubi, iliyopo Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, wamepiga kura za siri ili kuwafichua walimu wenye tabia ya kufanya mapenzi na wanafunzi wao shuleni hapo.

Uamuzi wa kupigwa kura hizo ulifikiwa hivi karibuni kwenye Kikao cha Baraza la Shule la Watoto ambacho kiliitishwa kwa lengo la kujadili vurugu zilizokuwa zikijitokeza shuleni hapo na kusababisha baadhi ya walimu kupigwa.

KIFO CHA MSANII ALBERT MANGWEA PIGO KWA TAIFA.









Wednesday, May 15, 2013

MITANDAO YA KIJAMII KAMA FACEBOOK UATHIRI WATU KISAIKOLOJIA- SOMA HAPA"








 
Facebook, mitandao mingine ya kijamii pamoja na huduma ya ‘blackberry mesenger’ maarufu kama BBM huathiri watu kisaikolojia, husababisha ndoa kuvunjika pamoja na usaliti katika uhusiano, wanasayansi wamebaini.

Utafiti huo uliofanywa mwaka 2012 na wanasayansi wa nchini Israel umebaini kuwa kwa wastani, wanawake wanatumia dakika 81 katika mitandao ya kijamii kwa siku ukilinganisha na wanaume ambao hutumia dakika 64, huku watu wasio na elimu wakionekana kuathirika zaidi na mitandao hiyo.

Friday, May 10, 2013

MAAJABU: PICHA ZA MIZOGA YA MBUZI NANE WACHINJWA MAKABURINI USIKU WA MANANE MOROGORO


Katika hali isiyo ya kawaida tumepokea taarifa kutoka kwa wafanyakazi  wa manispaa kitengo cha makaburi ya kolla wakidai kwamba usiku wa manane wa kuamkia juzii mbuzi nane wamechinjwa eneo la makaburi ya kola mkoani morogoro

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Wiliam Lukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya
Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha
Nne Mwaka 2012. 
Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011 ili Wanafunzi hao wawe katika mazingira yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka
iliyotangulia.

MAJINA 9 YA WATUHUMIWA WALIOLIPUA BOMU KANISANI-- ARUSHA


Imeripotiwa kuwa jumla ya watu 12 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa kutuhumiwa kuhusika na mlipuko wa bomu lililorushwa katika eneo la Kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi katika parokia teule ya Olasiti siku ya Jumapili, Mei 5, 2013 na kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 60.

Ripota wa WAPO FM radio alisema majina ya watuhumiwa hao yametajwa kuwa ni:-

  1. Victor Ambrose Calist (20, mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha)
  2. Joseph Yusuph Lomayani (18, mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha)
  3. George Bartholomeo Silayo (26, mkazi wa Olasiti, Arusha)

PICHA ZA MAZISHI YA WALIOKUFA KATIKA MLIPUKO WA BOM KATIKA KANISA LA MT JOSEPH ARUSHA.

Mapadri wa kanisa katoliki wakiwa wamebeba jeneza  lenyenye mwili wa mmoja wa waliokufa katika tukio la kutupwa kwa bomu la mkonokatika kanisa la Olasiti Arusha may 5, 2013. mazishi yaliyofanyika leo 

Thursday, May 9, 2013

HUYU NDIYE GAIDI ALIYERUSHA BOMU KANISANI, AFUNGA NA KUNENA MANENO MAZITO....SOMA HAPA..!!


Kijana aliyemkimbiza hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha akiwaelezea wananchi ilivyokuwa.



ALIYEMKIMBIZA hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha Jumapili iliyopita na kuua watu 3 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ameibuka.
Kijana huyo ambaye wakati akizungumza na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari jijini Arusha juzi alisahau kutaja jina lake, alisema kuwa shughuli ya kumnasa mtuhumiwa huyo haikuwa lelemama hata kidogo.

WANAFUNZI WA UMBWE SEKONDARI WAGOMA KULA KWA MADAI YA KUTORIDHISHWA NA MKUU WAO SHULE...!!

MGOGORO umeibuka katika Shule ya Sekondari Umbwe kati ya wanafunzi wa kidato cha tano na uongozi wa shule hiyo hali iliyosababisha baadhi ya wanafunzi kugoma kula na kufanya maandamano wakishinikiza kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa lengo la kutatua kero zilizoko shuleni hapo.
Kutokana na mgogoro huo, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Dk. Ibrahim Msengi aliyefika shuleni hapo kuutatua, alimtaka Ofisa Elimu Mkoa Kilimanjaro kupeleka wakaguzi katika shule

VIOJA VYA WANAFUNZI "KAMA HAKUNA NIDHAMU MASHULENI, MATOKEO YATAENDELEA KUFUTWA KILA MWAKA.....!!"




Kumekuwa  na   mvutano  mkubwa  kati  ya  wanataaluma  na  wanasiasa  kuhusu  suala  la  elimu  hapa  nchini.....
Wanataaluma  wengi  wanapinga  uamuzi  wa  serikali  kuyafuta  matokeo  ya  kidato  cha nne  kwa  madai  kwamba  hilo  siyo  suluhisho  la  la  tatizo ......

HII NDIO HALI YA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA WALIOJIUNGA NA JKT, ANGALIA MWONEKANO WA WAKIWA MAFUNZONI...!!



Hawa ni wanaume wakirushwa kichura na kamanda wa mafunzo, huko c mchezo......

VURUGU HUKO RUAHA WILAYA YA KILOSA

Taarifa nilizo zipata muda huu kutoka kwa mmoja wa wanakijiji cha Ruaha wilaya ya kilosa mkoani Morogoro zinaangaza kuwa kumetokea vurugu na mpaka muda huu mabomu yanarindima kila upande. Vurugu hizo zilizo sababisha kupigwa mabomu ni vurugu za kisiasa. 
Sababu za vurugu.
 
• Tarehe 24/4/2013 ulikuwa ufanyike uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji, mgombea wa Chadema alienguliwa na Afisa mtendaji wa kata ambaye ndiye alikuwa msimamizi wa uchaguzi.
 

ALIYEKUWA MHASIBU MKUU WA JAMBO LEO AFARIKI DUNIA



Aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, marehemu Vick Mgoyo
****************************************
MHASIBU Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts (T) Limited inayochapisha gazeti la Jambo Leo, Staa Spoti, Dar Metro na jarida la Jambo Brand Tanzania, Vicky Mgoyo (49), amefariki dunia.

Tuesday, May 7, 2013

TCU WAKIFUNGIA CHUO CHA KAMPALA INTERNATIONAL UNIVERSITY ( KIU ) KWA KUTOKIDHI VIGEZO

CHUO CHA KIU-DCC KUSIMAMISHWA KUTOA MAFUNZO YA SHAHADA ZA UZAMILI NA UZAMIVU


Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam (KIU-DCC) kilichopo Gongo la Mboto, Dar-Es-Salaam ni Chuo kilichopewa idhibati na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). Kufuatia kuendesha mafunzo ya shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) kinyume cha utaratibu na kutokua na wahadhiri wa kutosha wenye sifa stahili, Tume katika mkutano wake wa hivi karibuni ulikiamuru Kampala International University, Kampasi ya Dar-es-Salaam ifuatayo;
 

1. KIU isimamishe mara moja mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikiwa ni pamoja na Shahada za Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD) katika kampasi ya Dar-es-Salaam.
 

JESHI LA TANZANIA LIMESHATUA CONGO.....WAASI WA M23 WAANZA KUHAHA KWA KUJIKOSHA KWA WANANCH



Kwa mujibu wa mwandishi aliye na waasi  wa  m23, Diana Katabarwa kwenye Blog yake  anamnukuu kiongozi wa kisiasa wa M23  Mr. Bisimwa akiwambia wakazi wa North Kivu kuwa majeshi ya Tanzania na South Africa nimajeshi dhalimu yaliyo jaa rushwa na hayawezi kuibadili Congo....

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KANISA LA OLASITI ARUSHA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA KANISA PAMOJA NA WAUMINI.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Viongozi na Waumini wa Kanisa Katoliki la Olasiti Jijini Arusha May 7,2013 alikokwenda kutoa pole kufuatia mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono uliotokea kanisani hapo May 6,2013 na kusababisha vifo na majeruhi.

HATIMAYE BALOZI WA PAPA AONDOKA ARUSHA.



Mwakilishi wa Papa akiwa na Askofu Lebulu akitoka kwenye VIP ya Arusha Airport kuelekea kwenye ndege ya Precision .Ilikuwa ni dakika za majonzi na masikitiko kwa kundi lote lililokuwa limemsindikiza uwanja wa ndege Balozi wa Papa ambaye ameondoka leo mjini Arusha kuelekea Dar, baada ya kunusurika katika shambulio la bomu lililorushwa wakati akiwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi huko Olasiti Arusha.

NAY WA MITEGO AFANANISHWA NA DEM....CHID BENZ AMTUNGIA JINA NA KUMUITA " NEEMA WA MITEGO"

Ugomvi  wa  chini chini kati   ya Chid benz  na  Ney wa  mitego  sasa  umefikia  pabaya....
Juzi  Ney wa mitego  alionja  kichapo  toka  kwa  mashabiki  katika  show  yake  mbagala....Inadaiwa  kwamba Varangati hilo   lilitokana  na  madai  yake  kwamba   Chid  benz  ni  shoga  na  ametoboa  pua  kama  dem.... 

Mapema mchana huu Chidi Benz amefunguka kupitia ukurasa wake ya Facebook   na  kumtaka  NEEMA  WA  MITEGO(Neema ni jina la  kike )  aache  kumtukana  wala  kumwandika  message  zozote.....Vinginevyo  ataendelea  kuambulia  kichapo