Sunday, April 28, 2013

CHANGAMOTO ZA ELIMU: ELIMU POPOTE, CHAMSINGI KUELEWA



Kupata Elimu na maarifa katika mazingira yaliyoandaliwa vizuri ni changamoto sana kwa Waafrica. Katika Afrika hii kuna watu wanapata ELIMU kwa raha bila hata chengachenga za SHIDA au UGUMU wowote. Lakini pia kuna watu kwanza tu kuwahi kuona jengo lililojengwa kwa Tofali na kuwekewa sakafu ...hawajawahi kuona sembuse ubao na vifaa vyingine vya kujifunzia.

Hata hawa ni wanafunzi kama wanafunzi wengine wa mijini na mahali pengine popote na pia hata wao wanafanya mitihani hii hii wanaofanya wanafunzi wengine sijui ndo inaitwa NECTA EXAMINATION. Lakini cha ajabu utakuta wanauwezo wa kufahulu vizuri hata kuliko wanafunzi walioandaliwa katika mazingira mazuri ya kujifunzia.

No comments:

Post a Comment