Saturday, April 27, 2013

MH. LEMA KUFIKISHWA MHAKAMANI J'TATU

MAMBO yamezidi kumwendea Mrama Mbunge wa Arusha Mjini, (Chadema) Mheshimiwa Godbless Lema baada ya Jeshi la Polisi kutangaza rasmi kwamba itamfikisha Mahakamani, siku ya Jumatatu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amesema kwamba Mbunge huyo hawezi kuachiliwa huru kwa sababu mashtaka dhidi yake yameshakamilika na atafikishwa Mahakamani siku ya Jumatatau.

"Hatuwezi kumwachia kwa sababu anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili"alisema Sabas.

Wakati Kamanda huyo akitoa msimamo huo, taarifa za ndani za Jeshi hilo zinaeleza kwamba Mbunge huyo amehojiwa kwa zaidi ya saa nane sasa na bado yuko katika chumba maalum kwa mahojiano zaidi na maofisa wa Polisi huku akitakiwa kuonyesha ujumbe mfupi wa vitisho aliyodai kuwa ametumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.

Katika hatua nyingine,Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Arusha, kimekuwa na kikao kirefu kinachoongozwa na Mkuu wa Mkoa Mulongo na kwamba ajenda kubwa inayojadiliwa ni tukio zima la vurugu zilizotokea katika Chuo cha Uhasibu mkoani humo.

Lema alikamatwa usiku wa kuamkia jana baada ya Askari wa Jeshi la Polisi kumfuata nyumbani kwake na kuzingira nyumba yake kabla ya zoezi la kumchorpoa ndani ya nyumba hiyo kufanyika.

Mbune huyo anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kosa la kuchochea vurugu katika chuo hicho baada ya kutokea mauaji ya Mwanafunzi Henry Koga aliye uawa kwa kuchomwa kisu juzi akirejea chuoni hapo kutoka kwenye matembezi yake, hata hivyo haijajulikana mara moja sababu za kuawa kwa mwanafunzi huyo wala watuhumiwa hawajakamatwa.

No comments:

Post a Comment