Wednesday, April 24, 2013

TAKRIBANI WATU ZAIDI YA 100 WAFARIKI DUNIA BAADA YA GOROFA KUPOROMOKA BANGLADESH LEO

Jengo la gorofa nane lililokuwa na viwanda vya nguo na maduka limeporomoka leo mchana nje ya jiji la Dhaka, Bangladesh na kuuwa watu takribani 100 na kujeruhi watu wengine zaidi yaa 1000. Maafisa wa habari wa nchi hiyo wamesema vikosi vya uokoaji vinaendelea na shughuli ya kufukua vifusi ili kuweza kuopoa miili ya watu iliyofukiwa. TV imeonyesha wafanyakazi wanawake wakiokolewa na wengine walionekana wakiwa wamepoteza fahamu.

 Mmoja wa askari wa kikosi cha uokoaji alinukuliwa akisema kuwa katika jengo hilo walikuwako watu takribani 2000

No comments:

Post a Comment