PICHA YA MAREHEMU MUTULA KILONZO

Kiongozi huyu wa Makueni alifika nyumbani kwake siku ya Ijumaa mida ya saa kumi jioni akiwa anaendesha gari lake yeye mwenyewe. Na baada ya kufika alisalimiana na wafanya kazi wake na baada ya hapo kama ilivyo kawaida yake alitembelea ranch yake na kuona wanyama wake wakiwemo simba aliokua anawafuga katika Ranch yake. Wakati huo wafanyakazi wake walikuwa wakimuandalia chakula (Msosi) ambapo ilipofika mida ya saa moja usiku alipewa chakula na kula na baadae kwenda kulala katika chumba chake.
Ilipofika siku ya Jumamosi asubuhi wafanyakazi waliamka na kumuandalia chakula au Breakfast kama kawaida na kutenga tayari wakisubiri Boss wao Mutula Kilonzo aamke, lakini muda ulionekana unenda saa nne!!!......saa tano!!! na Boss huyo alikuwa haja aamka. Ndipo wafanyakazi wake wakaamua kwennda kumwamsha na dhani ni baada ya kuona sio kawaida yake kulala hadi mida hiyo.
Walifika katika chumba alicholuwa amelala na kugonga bila mafanikio ........baadae waliamua kuvunja mlango na kumkuta Mutula Kilonzo akiwa amelala na Povu likiwa linamtoka mdomoni. Na ndipo walipochukua hatua za kutoa taarifa panapo husika ili kuweza kupata msaada.
Na baada ya uchunguzi ikaonekana kuwa alikuwa ameshaaga Dunia muda mrefu.
Mutula Kilonzo hatuko nae tena
Pigo kwa FAMILIA YAKE
Pigo kwa TAIFA LA KENYA
Pigo kwa DUNIA NZIMA
KUTOKANA NA MCHANGO WAKE




hapo juu ni picha mbalimbali za waombolezaji wakiwemo viongozi wastaafu wa serikali ya Kenya.
Raila Odinga anaonekana akiwa katika huzuni kubwa sana pamoja na mwenzake Kalonzo Musyola.
No comments:
Post a Comment